Thursday 20 February 2025 - 15:01
Iran ndio nchi pekee katika eneo la kikanda ambayo imeweza kudumisha uhuru wake

Ayatollah Sayyid Yassin Mousawi amesisitiza kuwa, uongozi wa Iran katika nafasi ya mlezi wa kisheria ni Mwakilishi wa umma wa Imam Mahdi (a.t.f.s) na jukumu lake ni kuliongoza Taifa na kuliongoza kuelekea kwenye uadilifu na uhuru na akasema: Iran ndiyo nchi pekee katika eneo la kikanda ambayo imeweza kudumisha uhuru wake.

Kwa mujibu wa huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la "Hawza", Ayatollah Sayyid Yassin Mousawi, Profesa mashuhuri wa Seminari ya Najaf al-Ashraf, katika hotuba yake katika Shule ya Madina A-ilmu, alisisitiza umuhimu wa kutumia fursa zinazopatikana kwa Wairaq katika zama za sasa, na akasema: Fursa hizi huenda zisirudiwe tena. Alitoa mfano wa Hadithi ya Amirul-Muuminin Ali bin Abi Talib (amani iwe juu yake) ambapo alisema: "Faidikeni na fursa kwa sababu zinapita haraka kama mawingu."

Amesisitiza kuwa, fursa za hivi sasa zinazotolewa kwa Wairaq kuzungumza kwa uhuru kuhusu maslahi yao ya kidini na ya kidunia ni baraka (neema) inayopaswa kutumiwa.

Ayatollah Mousawi ameashiria kuwa, fursa hizo zilikuwepo kwa muda mfupi tu katika historia ya Iraq, kama vile enzi ya utawala wa kifalme na sehemu ya Jamhuri, lakini kutokana na kuingia madarakani kwa wakomunisti na dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyiwa nchini Iraq, fursa hizo zilitoweka.

Profesa wa Seminari ya Najaf al-Ashraf pia aliongeza kuwa Wairaq wengi, hasa kizazi cha vijana, hawajapitia kipindi hicho ambacho kulikuwa na fursa za kujifunza na kutoa maoni kwa uhuru.

Akigusia taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika eneo, Ayatollah Mousawi amesema: Mapinduzi haya yalikuwa ni mabadiliko makubwa yaliyosababisha waumini wa Iraq, Syria, Lebanon na nchi nyingine za Kiarabu kuiga mfano wake. Aliziita zama za sasa za Iraq "zama za kuundwa kwa mhimili wa upinzani (Muqawamah)" na kuongeza: Baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam Hussein, njia ilitengenezwa kwa ajili ya umoja wa waumini, Shia na Sunni. Madhumuni ya nguvu hizi ni kupinga tawala dhalimu.

Aidha alisema: Kituo kikuu cha nguvu duniani hivi sasa ni Marekani, lakini Iran ndiyo nchi pekee katika eneo la kikanda ambayo imeweza kudumisha uhuru wake na kupinga utawala wa Marekani.

Profesa wa seminari ya Najaf aidha ameongeza kuwa: Jukumu la Iran katika eneo la kikanda ni kuanzisha kikosi cha kuwalinda madhulumu duniani na kuyasaidia mataifa yenye imani kupata uhuru.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha